Polisi nchini Uganda imekikamata kikundi cha wanawake ambao walikuwa wanaandamana dhidi ya kuendelewa kushikiliwa kwa wame zao.
Wanawake hao, wengi wao wakiwa ni wanaharakati, wamesema kuwa haina maana kusherehekea Siku ya Wanawake Dunia bila wenzi wao.
Pia walielezea kusikitishwa sana na garama ya juu ya maisha.
Vyombo vya habari nchini Uganda vimesema kuwa wanawake hao walipelekwa katika kituo cha polisi, katika mji mkuu Kampala.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamewashutumu maafisa wa Uganda kwa kuwafunga mamia ya wakosoaji wa serikali kiholela. Vyombo vya habari vya Uganda vimeonyesha video za wanawake hao wakiandamana, huku wakiwa wameshikilia mabango ya ujumbe wao kwa serikali, kabla ya kukamatwa: