Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake wa Nigeria waliosafirishwa kwenda Libya waokolewa Niger

Wanawake Wa Nigeria Waliosafirishwa Kwenda Libya Waokolewa Niger Wanawake wa Nigeria waliosafirishwa kwenda Libya waokolewa Niger

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu nchini Nigeria linasema kuwa linachunguza hali iliyosababisha ulanguzi wa wanawake kumi na mmoja wa Nigeria kutoka nchini humo.

Waathiriwa waliokolewa katika nchi jirani ya Niger walipokuwa wakisafirishwa kuelekea Libya na kitengo cha biashara ya binadamu.

Waathiriwa ambao wote walikuwa vijana, walirejeshwa nchini Nigeria na kukabidhiwa kwa Wakala wa Kitaifa wa Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, (NAPTIP), huko Sokoto, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Kamanda wa NAPTIP Kanda ya Sokoto, Abubakar Tabra aliiambia BBC kwamba waathiriwa walipokelewa kutoka kwa maafisa wa Huduma ya Uhamiaji ya Nigeria, Kamandi ya Mpaka wa Illela mwishoni mwa juma lililopita, na wamehifadhiwa katika makazi yao salama wakiendelea na uchunguzi wa familia ili kuwezesha wasichana hao kuunganishwa na familia zao.

Maelezo ya waathiriwa yalionesha kuwa wanatoka zaidi kusini mwa Nigeria. Inasemekana waliibiwa simu na bidhaa zao katika vichaka vya Jamhuri ya Niger ambapo wafanyabiashara wao waliwatelekeza; kabla ya kuokolewa na Polisi wa Niger na kuwakabidhi maafisa wa uhamiaji wa Nigeria mpakani.

Chanzo: Bbc