Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake Sudan wafundishwa mafunzo ya kijeshi

Sudan Wanawake.png Wanawake Sudan wafundishwa mafunzo ya kijeshi

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake hao wamejiunga kwenye mafunzo maalumu yanayotolewa na serikali kwa lengo la kujikinga na mashambulizi na unyanyasaji wanaofanyiwa na vikosi vya msaada wa haraka la RSF, ikiwamo kubakwa.

Sudan. Taarifa kutoka nchini Sudan zinasema maelfu ya wanawake wa nchi hiyo wameamua kujiunga na jeshi ili kupata mafunzo kulisaidia kupambana na vikosi vya msaada wa haraka vya RSF.

Sambamba na hilo pia wanachukua mafunzo ya kujikinga na adui ambaye anadaiwa kuwanyanyasa wanawake hao ikiwemo kuwabaka. Kwa mujibu wa video iliyochapishwa na Al Jazeera.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu jeshi la nchi hiyo (SAF) likipambana vikali na vikosi hivyo vya RSF kwa kile kinachodaiwa kugombea madaraka.

Katika kutekeleza hilo wanawake hao sasa wanahudhuria kambi zilizoanzishwa na serikali ya nchi hiyo ikiwemo shule huko Port Sudan kwa ajili ya kujifunza jinsi ya kupigana na adui.

Wanafunzi, walimu na akina mama wa nyumbani wanakutana kila siku kujifunza mazoezi na jinsi ya kutumia bunduki aina ya AK47 kutoka kwa maofisa wa kijeshi.

Kwa upande mwingine, mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini humo, Mandeep O’Brien ameonya kuwa vita nchini humo vinahatarisha mustakabali wa raia wake milioni 24 wenye umri mdogo zaidi.

O’Brien ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na UN News na kuongeza kuwa "Sudan inakabiliwa na janga kubwa la kibinadamu lisiloelezeka. Ni jinamizi lililo hai kwa watoto.”

Mapigano hayo yaliyozuka Aprili mwaka jana yamesababisha watoto milioni 14 kukihitaji msaada wa kuokoa maisha yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live