Watu wanne wameaga dunia kufuatia mkanyagano wa saa tisa asubuhi katika lango la 'C' la uwanja wa Kericho Green siku ya Ijumaa.
Polisi walisema wanne hao walifariki walipokuwa wakipokea matibabu katika hospitali ya Rufaa ya kaunti.
Mkanyagano huo wa Siku ya Mashujaa ulisababishwa na bibi mmoja aliyekuwa akiuza chai nje ya uwanja huo ambaye kwa bahati mbaya alimwaga chai moto kwenye moto karibu na barabara ya umma.
Hii ilisababisha hofu ya umma ambayo ilidhaniwa kimakosa kuwa ni mabomu ya machozi yaliyorushwa kwao.
"Watu kadhaa waliotaka kuingia uwanjani walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kericho kwa gari la kituo na ambulensi za serikali ya kaunti," polisi walisema.