Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume Wakenya hutumia muda mwingi kujitunza kuliko wanawake - Ripoti

Wanaume Wakenya Hutumia Muda Mwingi Kujitunza Kuliko Wanawake   Ripoti Wanaume Wakenya hutumia muda mwingi kujitunza kuliko wanawake - Ripoti

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Wanaume wa Kenya hutumia muda mwingi kujitunza kuliko wanawake, ripoti imefichua.

Kulingana na ripoti ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya 2023, wanaume hutumia wastani wa dakika 710 kila siku kujitunza.

Hii hutafsiri kuwa takriban saa 11.83 kila siku ili kuhakikisha wanaonekana wamepambwa vizuri.

Wanawake kwa upande mwingine, hutumia takriban dakika 704.6 tu kujitunza. Hii inatafsiri kuwa masaa 11.73 kila siku.

"Muda unaotumika katika utamaduni, burudani, vyombo vya habari na shughuli za michezo ulikuwa wa juu zaidi kwa wanaume ikilinganishwa na wanawake," ripoti hiyo ilisoma.

Katika ngazi ya kitaifa, wanaume walitumia muda zaidi (dakika 158.1) kwa utamaduni, burudani, vyombo vya habari na mazoezi ya michezo ikilinganishwa na wanawake waliotumia dakika 118.8.

Muda unaotumiwa na wanaume kwenye shughuli zisizo za uzalishaji mali ulikuwa mkubwa zaidi mijini kwa dakika 67 kwa siku ikilinganishwa na dakika 57 katika maeneo ya vijijini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanawake wa maeneo ya vijijini walitumia muda mwingi katika shughuli zisizo za uzalishaji mali kwa dakika 282 kila siku ikilinganishwa na dakika 272 kwa wale wa mijini.

Katika ujamaa na mawasiliano, ushiriki wa jamii na mazoezi ya kidini, wanaume walitumia dakika 103.2 ikilinganishwa na wanawake waliotumia dakika 90.3.

"Kwa ujumla, muda uliotumiwa na wanaume kwa shughuli zisizo za Mfumo wa Uzalishaji wa Hesabu za Kitaifa (SNA) ulikuwa wa juu ikilinganishwa na wanawake katika kaunti zote na kinyume chake kinatumika kwa muda uliotumika katika shughuli zisizo za SNA," ripoti ya KNBS ilisema.

Jumla ya kaya 19,522 za sampuli zilibainika kustahiki uchunguzi huo. Kati ya kaya zinazostahiki, kaya 16,945 zilishiriki katika utafiti na kufanikiwa kujaza dodoso na kusababisha mwitikio wa kitaifa wa kaya wa asilimia 86.8.

Moduli ya matumizi ya muda ililenga watu walio na umri wa miaka 15 na zaidi. Kulikuwa na watu 40,764 waliostahiki moduli ya uchunguzi wa matumizi ya muda kutoka kwa kaya 16,945 zilizohojiwa.

Chanzo: Radio Jambo