Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume 60 waua nchini Burkina Faso

Wanaume 60 Waua Nchini Burkina Faso Wanaume 60 waua nchini Burkina Faso

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka kaskazini mwa Burkina Faso inasema takriban raia 60 wameuawa katika kijiji cha Karma, karibu na mpaka na Mali.

Mwendesha mashtaka wa eneo hilo alisema kuwa aliarifiwa kuhusu shambulio hilo siku ya Ijumaa, na kuongeza kuwa lilitekelezwa na watu waliokuwa wamevalia sare za jeshi.

Walionusurika wameliambia shirika la habari la AFP kuwa zaidi ya watu 100 waliokuwa kwenye pikipiki na lori walivamia kijiji hicho.

Mashambulizi dhidi ya jeshi la Burkinafaco na vikosi vya kujitolea yalifanyika katika eneo moja, karibu na Ouahigouya, mapema wiki iliyopita, na kusababisha vifo vya takriban 40 na zaidi ya 30 kujeruhiwa.

Maelfu ya watu wameuawa tangu wapiganaji wa Kiislamu waanze operesheni katika eneo hilo mwaka wa 2015.

Chanzo: Bbc