Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasiasa waliowekwa kizuizini Sudan waachiwa baada ya makubaliano

Gstjy Wanasiasa wa Sudan waliozuiliwa waachiliwa baada ya makubaliano

Mon, 22 Nov 2021 Chanzo: BBC

Majenerali tawala nchini Sudan wamewaachilia huru wanasiasa kadhaa raia waliokuwa wamezuiliwa baada ya mapinduzi ya mwezi uliopita.

Mkuu wa Chama cha Congress cha Sudan, Omar al-Degeir, aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa kwamba aliachiliwa Jumapili usiku kutoka kwa kifungo cha ndani, ambapo alikuwa ametengwa na ulimwengu wa nje.

Wanasiasa wengine, miongoni mwao kutoka chama kikuu cha Sudan, Umma, pia waliachiliwa huru.

Wajumbe wa serikali ya mpito iliyoondolewa wamekosoa vikali makubaliano ya Jumapili ya kumrejesha madarakani Waziri Mkuu Abdalla Hamdok na kuyataja kuwa ni usaliti.

Wakosoaji wana mashaka kuwa jeshi litamruhusu yeye na baraza lake la mawaziri la wanateknolojia kushikilia mamlaka ya kweli.

Chanzo: BBC