Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasiasa bandia wanasajili wanajihadi - rais wa Msumbiji

Wanasiasa Bandia Wanasajili Wanajihadi   Rais Wa Msumbiji Wanasiasa bandia wanasajili wanajihadi - rais wa Msumbiji

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amesema kuna watu wanaojifanya wanasiasa ili kuwasajili vijana katika safu ya wanamgambo wa jihadi.

Wanamgambo hao wamekuwa wakiendesha mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo tangu mwaka 2017. Akizungumza katika sherehe za kuhitimu kijeshi, rais aliongeza kuwa serikali inafahamu kuhusu jambo hilo na wale watakaobainika kuhusika watahukumiwa na kuhukumiwa.

“Watu hao, tunapowakamata, mahali pao ni jela,” Bw Nyusi alisema.

Pia alisisitiza kwamba jeshi lake lilikuwa likifanya harakati fulani dhidi ya wanamgambo hao kaskazini mwa nchi, jambo ambalo limesababisha kukamatwa kwa baadhi ya wanajihadi na viongozi wao, pamoja na silaha walizotumia.

Chanzo: Bbc