Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasiasa ambao kwa sasa wanakula kwenye meza moja na DP Ruto

A66c6ed9c2ffde04 Wanasiasa ambao kwa sasa wanakula kwenye meza moja na DP Ruto

Wed, 29 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Chama cha UDA kimewavutia wanasiasa wengi hasa wale waliokuwa kwenye chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru KenyattaBaadhi ya wanasiasa hao ni Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, Gathoni Wa Muchomba, Cate Waruguru, Majimbo Kalasinga, na Gavana wa Migori Okoth ObadoIdadi kubwa ya wanasiasa humu nchini wamekimbilia kambi ya Naibu Rais William Ruto huku siasa na kampeni za uchaguzi mkuu wa 2022 zikishika moto.

Wengi wa wanasiasa hao wanatafuta vyama watakavyovitumia kutetea viti vyao ifikapo 2022.

Naibu Rais William Ruto ambaye alikihama chama cha Jubilee mapema mwaka huu, ametangaza kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama chake kipya cha UDA.

Hata Hivyo, chama cha UDA bila shaka kimewavutia wanasiasa kadhaa hasa wale waliokuwa kwenye chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

TUKO.co.ke iliweza kukuandalia orodha ya majina ya wanasiasa ambao kwa sasa wanakula kwenye meza moja na DP Ruto;

1. Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru

Kabla ya kujiunga na chama cha UDA majuma kadhaa yaliopita, Waiguru alikiri kwamba chama cha Jubilee kimekufa na atakuwa anafanya makosa makubwa kukitetea kiti chake kupitia tiketi ya chama hicho.



Waiguru alidai kwamba aliwauliza wakazi wa Kirinyaga kuhusu chama walichotaka kujiunga nacho na wakapendekeza chama cha Ruto cha UDA.

“Nilisema nitafanya vile watu wa Kirinyaga wanataka. Nataka niwaulize mnataka nikuje na chama gani huku Kirinyaga ili mnirudishe? Waiguru aliuliza.

“Nikikuja na hio chama mtanirudisha? Mimi nitasema si mimi nilisema, nimeuliza wananchi na nitafanya vile wanasema,” alisema Waiguru baada ya kuarifiwa ajiunge na UDA.

2. Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kiambu Gathoni Wa MuchombaWa Muchomba ambaye alikuwa katika mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kieleweke katika chama cha Jubilee alihiari kuabiri wilbaro Juni 23, 2021.

Mbunge huyo alisema alishauriwa na wakazi wa Kiambu kujiunga na chama cha UDA.

" Baadaya kufanya mashauriano na wakazi wa Kiambu, nimefanya uamuzi kukiondokea chama ambacho kilinipeleka bungeni na kujiunga na kile ambacho watu wangu wanakitaka," Alisema Wa Muchomba.

3. Mwakilishi wa wanawake wa Laikipia Cate WaruguruMbunge Cate Waruguru alidai kwamba chama cha Jubilee kilikuwa kinaelekea kufa na juhudi za kukikomboa zilikuwa duni sana.

Alisema hii ni kutokana na matokeo duni ambayo Jubilee ilipata katika chaguzi ndogo za eneo bunge la Juja na Kiambaa ambapo chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Ruto kilishinda.

"Tuna shida kubwa na sidhani tutakomboa chama chetu kabla ya rifarenda na uchaguzi mkuu ujao wa 2022," alisema.

"Ninatangazia chama...endapo mambo hayatafanya kazi watu wangu wamenishauri kile natakiwa kufanya" alisema Waruguru.

4. Mbunge wa Kabuchai Majimbo KalasingaMiezi sita baada ya Majimbo kuchaguliwa mbunge wa Kabuchai kwa tiketi ya chama cha Ford- Kenya, mwanasiasa huyo alikihamia chama cha UDA akidai huko ndiko anajihisi kuwa nyumbani.

Akitangaza kukihamia chama hicho, Majimbo alimshukuru Ruto kwa kuchangia pakubwa ushindi wake wa kuwa mbunge.

" Mpendwa Naibu Rais, ningependa kukufahamisha kwamba wewe na kaunti ya Bungoma ni kitu kimoja na tuko tayari kufanya kazi kwa pamoja na wewe ili uwawezeshe hustlers wa nchii hii," Majimbo alisema.

5. Gavana wa Migori Okoth ObadoBaada ya gavana Obado kutofautiana na viongozi wa chama cha ODM, Obado alikuunda chama chake kipya cha People’s Democratic Party (PDP).

Hata hivyo, Obado ametangaza rasmi kwamba yuko tayari kuunda muungano na chama cha UDA.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke