Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasiasa 24 wameajiandikisha kugombea urais DRC

Drc Urais 24.jpeg Wanasiasa 24 wameajiandikisha kugombea urais DRC

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo imetangaza kuwa, imepokea fomu za wagombea 24 wa urais ambao wamejisajili kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika Desemba 20 mwaka huu.

Licha ya orodha hiyo, wagombea bado wanahitaji kuidhinishwa na mahakama ya kikatiba kabla ya orodha kamili ya wagombea kuchapishwa tarehe 18 ya mwezi ujao wa Novemba.

Rais Felix Tshisekedi, aliyeingia madarakani mwaka wa 2018, amewasilisha ombi la lake la kuwania katika uchaguzi huo mapema mwezi Oktoba, akiwania kuongoza DRC kwa awamu ya pili.

Licha ya kuweko idadi kubwa ya wagombea, lakini mchuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya Kiongozi mwandamizi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Martin Fayulu na Rais Felix Tshisekedi.

Fayulu alinukuliwa hivi karibuni akisema: "Tutaendelea kupigania uwazi katika uchaguzi. Hatukupata fursa ya kukagua daftari la wapiga kura lakini tutakuwa macho wakati wa upigaji kura",

Martin Fayulu na Felix Tshisekedi

Aidha mpinzani huyo anasema, ushindi wake uliibwa wakati wa uchaguzi wa rais wa Desemba 2018 ambapo Tshisekedi alitangazwa mshinidi.

Utawala wa Rais Tshisekedi umekumbwa na hali ngumu ya uchumi, janga la Covid 19, mlipuko wa Ebola, ukosefu wa usalama hasa mashariki ya nchi ambako wapiganaji wa kundi la M23 waliteka sehemu ya maeneo ya mashariki na kusababisha kuvunjika kwa uhusiano na Rwanda.

Felix Tshisekedi, kijana wa mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Etienne Tshisekedi, aliyeahidi kupambana na ulaji rushwa na utawala wa kimabavu anakanusha tuhuma kutoka makundi ya kutetea haki za binadama na wakosowaji wake, kwamba ameshindwa kutekeleza ahadi zake.

DRC yenye utajiri wa maliasili, ni nchi ya 10 maskini zaidi duniani ambapo 77.2% ya wakazi wake wanaishi kwa dola 1.9 kwa siku, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live