Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasheria wakomalia kauli ya Jaji Maraga

E632aec225125f8235a0c58a17feb7ac Wanasheria wakomalia kauli ya Jaji Maraga

Tue, 29 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Wanasheria Kenya (LSK) kimesema Rais Uhuru Kenyatta hawezi kulazimishwa kutekeleza ushauri wa Jaji Mkuu, David Maraga wa kulivunja Bunge wakati huu, kwa sababu kiongozi huyo wa nchi ana muda wa hadi Oktoba 12 kutekeleza ushauri huo.

Chama hicho kimesema itakapofika tarehe hiyo endapo Rais Kenyatta atakuwa hajatekeleza ushauri huo, yapo mambo kadhaa yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kutekeleza ushauri huo au kulazimisha hatua fulani kuchukuliwa.

“Kama hadi Oktoba 12 Rais Kenyatta atakuwa hajatekeleza ushauri wa Jaji Maraga, wabunge wote wanatakiwa kusimamishwa mishahara yao, kuwaondolea ulinzi na kufungwa rasmi shughuli zote za kibunge,” alisema Rais wa LSK, Nelson Havi.

Kwa mujibu wa chama hicho, baada ya hatua zote hizo kuchukuliwa, hatua inayofuata itakuwa ni kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutangaza uchaguzi mkuu katika kipindi kisichozidi siku 90 na watakaochaguliwa watatumikia nafasi hizo katika kipindi kilichosalia tu kabla ya uchaguzi mkuu unaofuata.

Chama hicho kilisema ikiwa Rais Kenyatta hatatekeleza ushauri huo katika muda unaotakiwa, atakuwa amevunja Katiba ya nchi na kuanzia wakati huo Bunge litakuwa sio halali tena kufanya kazi za kibunge.

“Kwa kazi yoyote itakayofanywa na wabunge wakati nchi ikiwa katika hali

Chanzo: habarileo.co.tz