Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasayansi huenda wamegundua jinsi piramidi za Misri zilivyojengwa

Wanasayansi Huenda Wamegundua Jinsi Piramidi Za Misri Zilivyojengwa Wanasayansi huenda wamegundua jinsi piramidi za Misri zilivyojengwa

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Bbc

Wanasayansi wanaamini kuwa huenda wamefumbua fumbo la jinsi piramidi 31, ikiwa ni pamoja na jumba maarufu duniani la Giza, zilivyojengwa nchini Misri zaidi ya miaka 4,000 iliyopita.

Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha North Carolina Wilmington imegundua kwamba piramidi hizo huenda zilijengwa kando ya mkondo wa Mto Nile uliopotea kwa muda mrefu - ambao sasa umefichwa chini ya jangwa na mashamba.

Kwa miaka mingi, wanaakiolojia wamefikiri kwamba Wamisri wa kale lazima walitumia njia ya maji iliyo karibu kusafirisha vifaa kama vile mawe yaliyohitajika kujenga piramidi kwenye mto huo.

Lakini hadi sasa, "hakuna mtu aliyekuwa na uhakika wa eneo, umbo, ukubwa au ukaribu wa njia hii kubwa ya maji hadi eneo halisi la piramidi", kulingana na mmoja wa waandishi wa utafiti huo, Prof Eman Ghoneim.

Katika juhudi za kuvuka bara zima, kikundi cha watafiti kilitumia picha za satelaiti za rada, ramani za kihistoria, uchunguzi wa kijiofizikia, na uwekaji wa mashapo (mbinu inayotumiwa na wanaakiolojia kupata ushahidi kutoka kwa sampuli) kuchora mkondo wa mto - ambao wanaamini lilizikwa na ukame mkubwa na dhoruba za mchanga maelfu ya miaka iliyopita.

Timu hiyo iliweza "kupenya uso wa mchanga na kutoa picha za vipengele vilivyofichwa" kwa kutumia teknolojia ya rada, utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Nature, ulisema.

Miongoni mwa vipengele hivyo ni "mito iliyozikwa na miundo ya kale" inayotembea chini ya vilima ambapo "idadi kubwa ya piramidi za Kale za Misri ziko," Prof Ghoneim alisema.

Chanzo: Bbc