Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaojiuza wakabidhiwa Tsh. Milioni 20 walizoahidiwa na Naibu Rais Ruto

A2e4a76784112fd9 Makahaba wakabidhiwa Tsh. Milioni 20 walizoahidiwa na Naibu Rais Ruto

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wanaojiuza kutoka mitaa ya Mtito Andei nchini Kenya, katika Kaunti ya Makueni walioahidiwa shilingi milioni 20 na Naibu Rais William Ruto, hatimaye wamepokea fedha hizo.

Makahaba hao wameonesha furaha yao jinsi Ruto alivyowakumbuka na kusema ni Yesu tu aliyewahi kuchukua muda wake kuwasaidia makahaba duniani. Walisema kati ya Marais wanne wa nchi hii, ni Naibu Rais pekee ndiye aliyeweza kutambua kazi yao na kuwahimiza kufanya kazi nyingine nadhifu.

Makahaba hao walidokeza kwamba tayari wamefanya uchunguzi ni biashara gani wataanzisha na fedha hizo.

Makahaba hao walipokea hela hizo siku ya Jumapili Disemba 5.

“Tumefurahia kwamba Naibu Rais ametukumbuka. Ni Yesu tu aliyewahi kuchukua muda wake na kuwasaidia makahaba,” mmoja wa makahaba hao alisema.

Alisema kwamba kati ya marais wanne wakiwemo; Mzee Jomo Kenyatta, Daniel Moi , Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta, ni Naibu Rais Ruto ndiye aliyeamua kutambua kazi yao na kuwahimiza kuanza kufanya biashara nyingine bora zaidi.

Kahaba mwingine alisema ilimbidi kuchukua mapumziko mafupi kususi amshukuru Ruto kwa kuwazawadi pesa hizo. Alisema tayari wamesikilizana ni biashara ipi watakayoanzisha.

“Tutajihusisha na biashara ya table banking. Tutanunua hema na viti ili tuzikodihe kwa watu,” kichuna huyo alisema.

Akihutubu kwenye mkutano wa siasa eneo la Makueni, mnamo Oktoba 26, DP Ruto aliwataka wanawake hao kubuni chama ili waweze kupokea fedha hizo.

Ruto aliombwa kutenga kisasi fulani cha fedha na mmoja wa makahaba hao kutoka kwa ‘hazina ya kuwawezesha mahasla’ ili waweze kufungua biashara nadhifu.

Naibu Rais alisema atakuwa nawafuatilia makahaba hao, ili kuhakikisha wameanzisha biashara nyingine bora na pesa hizo alizowapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live