Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananwake Tunisia wakabiliwa na ukatili mkubwa

Tunisia Ukatili Kijinsia Wananwake Tunisia wakabiliwa na ukatili mkubwa

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wa Tunisia wanakabiliwa na hali mbaya ya ongezeko la ukatili na mauaji dhidi yao yanayofanywa na waume zao au na ndugu wa familia zao.

Mashirika ya haki za binadamu nchini Tunisia yametangaza kuwa, idadi ya wanawake waliouawa katika mikoa tofauti nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2023 imefikia watu 9.

Idadi ya vifo mtawalia vya wanawake huko Tunisia vinaongezeka katika kiwango cha kushtusha licha ya nchi hiyo kutambulika kama kinara wa kuheshimu haki za wanawake miongoni mwa nchi za Kiarabu.

Watetezi wa haki za binadamu huko Tunisia wamelaani utekelezaji dhaifu wa mahakama wa sheria namba 58 ya mwaka 2007 na kushindwa kuchukua hatua viongozi wa vyombo vya usalama na mamlaka husika za nchi hiyo ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

Ahlam al Hamami mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Tunisia anasema kuwa: Mauaji ya wanawake huko Tunisia yanatisha kufuatia kujiri visa 9 vya mauaji katika miezi mitatu iliyopita. Amesema kiwango hiki cha mauaji kinaonyesha kuwa kiujumla vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake nchini humo vimeongezeka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live