Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa Watupwa Jela kwa Kutesa Mtoto Wao wa Kumzaa

JELA2 Wanandoa Watupwa Jela kwa Kutesa Mtoto Wao wa Kumzaa

Sat, 11 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAUME mmoja na mke wake wa pili wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusababisha madhara mtoto wao wa kuzaa kwa kipigo.

Joseph Ireri Njeru mwenye umri wa miaka 42, na Bi. Bancy Wanja Nyaga 30, wanaotoka kijiji cha Njakairi kaunti ya Embu huko nchini Kenya.

Wawili hao wanasemekana kumtesa na kumjeruhi vibaya mtoto wao mwenye umri wamiaka 9 kwa kumuadhibu kwa namna ya isiyo ya kawaida kwa kosa la kwenda kumtembelea bibi yake kinyume cha matakwa ya wazazi wake.

Inaelezewa Julai 2, 2021, wazazi hao walimfunga mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 kwenye kiti cha sofa, na kumchapa viboko mara kwa mara kwa kutumia kamba ngumu ilikuwa ikitumika kumfunga Mbwa.

Na baada ya kufanya kitendo hicho, walimwagia maji ya baridi akiwa kwenye kiti hicho na kumuacha hapo kwa muda wa siku mbili mfululizo.

Ndugu wa mtoto huyo baadaye walimkomboa kutoka kwenye kiti hicho, kitendo kilichowaingiza matatani baada ya wazazi wao kubaini kitendo cha wao kumfungulia mdogo wao, hivyo nao wakaadhibiwa vikali kwa kosa la kumuokoa mtoto huyo.

Baadaye mjomba wa watoto hao aliingilia kati na kuwasilisha malalamiko juu ya matukio hayo katika kituo cha polisi kilicho karibu kitendo kilichopelekea wanandoa hao kutiwa mbaroni.

Mke wa kwanza (Bi mkubwa) wa mwanaume huyo, aliamua kuihama nyumba baada ya kutokukubaliana na adhabu aliyokuwa anaipata mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live