Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wasiooga wapigwa marufuku kuingia mjini

Kuoga Maji Baridi.png Wananchi wasiooga wapigwa marufuku kuingia mjini

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA) nchinin Uganda imeripotiwa kuwa mbioni kuanzisha sera mpya ambayo itawahitaji raia wa nchi hiyo kuoga kabla ya kuingia mjini.

Raia wa Uganda watalazimika kuoga kabla ya kuingia katika Jiji la Kampala iwapo sera hiyo mpya itapitishwa.

Taarifa zimedokeza kwamba Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA) imebuni sera hiyo baada ya kubaini kuwa harufu ya kimwili husababisha uchafuzi wa hewa.

Wanasayansi wanaoratibu sera hiyo wanaamini kuwa hatua hiyo itaboresha kwa kiwango kikubwa hali ya hewa katika Jiji la Kampala.

Mtandao wa Tuko umeeleza kwamba chanzo cha uhakika kutoka ndani ya mamlaka hiyo, kilidokeza kuwa hatua hiyo inalenga kusafisha hewa katika jiji hilo baada ya ripoti ya hivi karibuni kuonyesha kuwa harufu ya mwili ndio chanzo kuu cha uchafuzi wa hewa katika jiji hilo.

Ameeleza kuwa wanasayansi wa mazingira wa mamlaka hiyo walifanya uchunguzi wa kina na pia waliwahoji watu jijini humo kabla ya kuafikia uamuzi huo wa kusafisha hewa jijini Kampala kwa kuwalazimisha watu kuoga. "Tumejenga vituo 24 vya kuoga kwenye barabara kuu zote zinazoingia jijini. Itakuwa ni lazima kwa watu kuoga kabla ya kuingia Kampala au watazuiwa kuingia jiji," kiliieleza chanzo hicho na kuongeza,

"Ikiwa mtu ataoga sehemu yoyote atapewa kibali cha siku moja cha kuingia jijini Kampala, na atalazimika kufanya vivyo hivyo siku nyingine."

Kupitishwa kwa sera hiyo kutaifanya Kampala kuwa jiji la kwanza duniani kutekeleza sera inayohitaji watu kuoga kabla ya kufika mjini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live