Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wajawa hofu thibitisho la uwepo wa Ebola

220920050631 Uganda Declares Ebola Outbreak Intl 1140x640 Wananchi wajawa hofu thibitisho la uwepo wa Ebola

Wed, 21 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa nchi ya Uganda na maeneo ya jirani wameingia hofu baada Serikali ya nchi hiyo kuthibitisha kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola (EVD) na uwepo wa taarifa ya kifo cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa wilaya ya Mubende, iliyoko kilomita 150 magharibi mwa mji mkuu Kampala, ambaye aliaga dunia Septemba 19, 2022 kwa kuugua maradhi hayo.

Akizungumza na vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Uganda, Dkt. Diana Atwine alitoa maelezo zaidi kwamba mgonjwa aliyeporipoti hospitalini, alikuwa na dalili zinazoshukiwa kuwa ni za Ebola ambaye alitengwa na sampuli ilichukuliwa Septemba 18, 2022 na matokeo yake kutolewa jioni ya Septemba 19, 2022, kuthibitisha kuwa alikuwa na ugonjwa wa Ebola, aina ya Sudan.

Uthibitisho huo, unafuatia uchunguzi wa timu ya mwatabibu wa Taifa ya Majibu ya Haraka kuhusu vifo vinavyotiliwa shaka vilivyotokea wilayani humo mwezi huu, ambapo Dkt. Atwine amesema, “Katika kijiji hicho hapo awali tumepata taarifa kuhusiana na vifo vya jamii, ambavyo wataalam wetu wa magonjwa walikwenda kubaini.”

Ameongeza kuwa, “Kwa bahati nzuri, hawakuthibitishwa, walizikwa. Walakini, muundo ulikuwa ndani ya familia moja watu wazima watatu na watoto watatu.” huku shirika la Afya Ulimwenguni WHO likisema washukiwa wanane kwa sasa wanapokea huduma katika kituo cha afya.

Hata hivyo, Dkt. Diana Atwine amewataka wananchi kuwa watulivu, huku akiwasifia wataalamu wa Uganda kwamba, “Tuna uwezo, tuna ujuzi, tunacho kinahitajika ili kudhibiti ugonjwa huu wa Ebola… kwa hiyo tunawaomba watulie na kuwajulisha. kwamba tutashughulikia janga hili kwa usahihi.”

Ebola huenea kwa kugusana moja kwa moja na damu, viungo au majimaji mengine ya mwili ya watu walioambukizwa, popo na kula nyama ya nyani au kutumia vitu kwa kuchangia na mgonjwa aliye na maambukizi na tayari Mamlaka nchini DR Congo iliyo jirani na Uganda ikisema Agosti, 2022 kisa kipya cha virusi hivyo kilihusishwa na mlipuko wa hapo awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live