Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wahoji sababu za Rais kutumia Tsh. Bilioni 9.5 kwenye mkutano wa "UNGA"

Angola Presidenta Bajeti ya safari ya Rais wa Angola yawa gumzo

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asasi za kiraia pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa nchini Angola wamekosoa safari Rais João Loureço ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 76 wa Wakuu wa nchi uliofanyikia mjini New York wakidai kuwa na matumizi makubwa ya kifedha.

Mnamo Septemba 8 mwaka 2021, Rais huyo aliidhinisha jumla ya dola za kimarekani milioni 4.11 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 9.5 kutumika kama gharama atakazotumia katika kikao hicho kilichomalizika tarehe 24, septemba , 2021.

Kinyume na ahadi zake, Rais huyo aliyeingia madarakani Septemba, 2017 alihaidi kupambana na vitendo vyote vya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za Umma katika uongozi wake ili kujenga uchumi wa taifa hilo.

Wakosoaji hao wamelalamikia gharama hizo kuwa ni kubwa hasa katika kipindi hichi ambacho taifa hilo linapambana kunusuru uchumi ulioharibiwa na ugonjwa Corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live