Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wa Tunisia wataka kufukuzwa balozi wa Marekani

AF46926F 64EF 4AE4 8F22 8DE2E27D1B00.jpeg Wananchi wa Tunisia wataka kufukuzwa balozi wa Marekani nchini mwao

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya raia wa Tunisia wameandamana na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani nchini humo, wakipinga kuendelea kuuawa kwa raia katika Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wametoa mwito wa kufukuzwa nchini humo balozi Marekani.

Wanaharakati ambao ni wanachama wa "hatua za Pamoja Kwa Ajili ya Palestina" na Mtandao wa Tunisia wa Kukabiliana na Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Israel" walifanya maandamano na mkusanyiko huo licha ya hatua za vyombo vya usalama za kuwazuia kwa kisingizio cha vitisho vya usalama.

Baada ya kukusanyika mbele mbele ya Ubalozi wa Marekani nchini Tunisia na kuimba. nara, Amerika inayoshiriki imelaani uchokoz waliisikika wakitoa nara za kulaani jinai za Israel huko Gaza na kuitaja Marekani kuwa mshirika wa jinai hizo na kutaka balozi wa Marekani afukuzwe kutoka Tunisia.

Maandamano ya wananchi wa Tunisia ya kuunga mkono Palestina

Kwenye maandamano hayo, wananchi wa Tunisia wamesikika wakitoa matamshi kwa sauti kubwa, ya kulaani siasa za kibeberu za Marekani, wamepaza sauti zao kuliunga mkono taifa madhlumu la Palestina kama ambavyo wamesikika pia wakitangaza kwa sauti kubwa kwamba rais wa Marekani, Joe Biden ni mtenda jinai.

Ikumbwe kuwa, wananchi wa Tunisia wamekuwa wakimiminika mabarabarani mara kwa mara kufanya maaandamano ya kulaani jinai zinazoendelea za Marekani kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Gaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live