Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wa Morocco waandamana kulalamikia gharama kubwa za maisha

Maandamano Morocco.jpeg Wananchi wa Morocco waandamana kulalamikia gharama za maisha

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Morocco jana usiku waliandamana katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kupinga kupanda pakubwa kwa bei za bidhaa za chakula. Maandamano hayo yamefanyika kufuatia wito uliotolewa na muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto nchini humo.

Huko Casablanca, wakazi wa mji huo waliandamana kupinga kuanda sana kwa bei za vyakula. Wamesema maisha yamekuwa machungu kutokana na gharama kubwa za vyakula vya mahitajio.

Wafanyamaandamano hao wa Morocco wamekosoa sera za serikali ya nchi hiyo ambayo iliwaahidi kuwa itakuwa serikali ya kijamii lakini badala yake wanashuhudia kuwepo kwa matabaka na kukosekana kwa uadilifu katika jamii. Wakazi wa miji ya Rabat, Tangier na Marrakech pia jana usiku waliandamana kupinga kupanda kwa bei za vyakula huko Morocco.

Makumi ya raia wa Morocco ambao wameandamana mbele ya Bunge la nchi hiyo wameeleza kuwa kupanda kwa bei za vyakula nchini humo kunatia aibu. "Nchi yetu ni ya kilimo lakini bidhaa aina ya mboga zinauzwa ghali sana", wamesema.

Maandamano hayo yameripotiwa huko Morocco huku kukiwa na ongezeko la mfumuko wa bei ambao umeiweka serikali ya nchi hiyo chini ya mashinikizo ya vyama vya wafanyakazi, wapinzani na vyombo vya habari vya ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live