Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Zambia wakiona cha Moto

Zambia Deploys Army To Curb Violence Ahead Of Polls Jeshi laingia Mtaani nchini Zambia

Mon, 2 Aug 2021 Chanzo: DW

Rais wa Zambia Edgar Lungu amesema ameamuru jeshi kuingia mitaani kumaliza machufuko yanayoshuhudiwa kuelekea uchaguzi mkuu wa taifa hilo uliopangwa kufanyika Agosti 12.

Rais Lungu amesema ili kuimarisha utii wa sheria na kukomesha machafuko ya kisiasa yaliyoshuhudiwa katika muda wa siku mbili zilizopita wanajeshi wanapelekwa mitaani kuwasaidia polisi kuimarisha hali ya usalama.

Katika viunga vya mji mkuu, Lusaka na majimbo mengine nchini Zambia wafuasi wa chama tawala cha Patriotic Front na wale wa chama kikuu cha upinzani cha UPND wamepambana kwa mapanga, mashoka na silaha nyingine.

Licha ya tume za uchaguzi kupiga marufuku mikutano ya kampeni kama sehemu ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corpna makabiliano baina ya wafuasi wa vyama vya siasa yameongezeka na kuwazidi nguvu polisi.

Hatua ya rais kuwatumia wanajeshi, imetokana na mauaji ya wafuasi wawili wa chama tawala katika mji mkuu Lusaka, akisema hawezi kuruhusu kutokea tena kwa mauaji kama hayo kwengineko nchini.

Chanzo: DW