Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Libya wahoji juu ya kuachiwa kwa mtoto wa Gaddafi

Daadfire.jpeg Saadi Kadhafi, mtoto wa Muammar Gaddafi

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wananchi nchini Libya wamehoji juu ya kuachiwa kwa Saadi Kadhafi, Mtoto wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, aliyekuwa akitumikia kifungo kwa takribani miaka minne.

Wengi wameonesha kutofurahia uamuzi huo wakiamini ni kuchichea vuguvugu jipya la vurugu kwa kile wanachoamini kuwa maamuzi hayo sio ya manufaa kwao.

"Kwanini Sadadi na Ahmad Ramadan(afisa usalama)waachiwe katika kipindi hiki? hii inaonesha dhahiri kuwa siasa inahusika katika hili"Abdellatif Dakdak mmoja Mmoja wa wadau nchini humo.

Katika kila jambo, kuna mapokeoa ya aina mbili, wapo walifurahia maamuzi hayo kwa kuamini kuw ani mwanzo mzuri wa kujengaSerikali yenye weledi wa kupambana na majanga yanayoikumba nchi hiyo.

"Kilichotokea kinadhihirisha wazi kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha, na hakuna aliyejuu ya sheria, Mahakama imefikia maamuzi baada yakujidhirisha na hii inaonesha kuwa kuna usawa na haki inatendeka" Mohammed Ali Jawaylak

Saadi alikamatwa kwa makosa ya mauaji akihusishwa kuwafyatulia risasi waandamanaji, na kabla ya kukamatwa alikuwa akijishughulisha na uchezaji wa mpira akitumikia timu ya taifa ya nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live