Mamlaka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wamemuua mhandisi na walinzi watatu kutoka Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga.
Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira ya Congo (ICCN) ilisema watu wenye silaha, wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa Mai Mai, walishambulia msafara wa wafanyakazi wake siku ya Alhamisi asubuhi.
Virunga ndio hifadhi ya zamani zaidi barani Afrika na hifadhi maarufu ya wanyama adimu, kama vile sokwe wa milimani.
Pia imekuwa maficho ya wanamgambo wa Mai Mai.
Makundi ya waasi mbalimbali wenye silaha wamekuwepo kwenye eneo la Congo mashariki kwa miongo kadhaa.