Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kiislamu waua watu 10 Burkina Faso

Wanamgambo Wanaoshukiwa Kuwa Wa Kiislamu Waua Watu 10 Burkina Faso Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kiislamu waua watu 10 Burkina Faso

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: Voa

Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso Jumanne alikemea“ukatili’’ wa wanamgambo wa Kiislamu wa nchi hiyo baada ya vyanzo vya ndani na vya usalama kuripoti vifo vya raia 10 katika mashambulio mawili.

Wakazi wa Nouna, mji wa mkoa wa Kossi magharibi mwa nchi, walioawasiliana kwa simu na shirika la habari la AFP, wamesema mji huo ulishambuliwa kwa makombora Jumatatu jioni.

Mkazi mmoja amesema “watu sita walikufa na wanne kujeruhiwa.”

Mji wa Nouna ulipokea katika miezi ya karibuni maelfu ya watu waliokimbia mashambulizi ya mara kwa mara ya wanamgambo wa kiislamu kwenye makazi yao.

Chanzo cha usalama kimeithibitishia AFP shambulio la Nouna, na kusema “mabaki ya roketi yalipatikana katika eneo hilo.”

Jioni hiyo hiyo, kwenye umbali wa kilomita 400 kusini mwa nchi, mji wa Tondoura ulio karibu na mpaka wa Ivory Coast, ulishambuliwa pia, chanzo kimoja ambacho hakikutaka jina lake litajwe kimeiambia AFP.

Chanzo hicho kimesema” magaidi walishambulia kijiji. Baadhi ya wanakijiji, wakiwa na bunduki, walijaribu kuingilia kati lakini walivamiwa haraka.”

Chanzo: Voa