Wanamgambo wa kiislamu waliwakata vichwa wakulima 10 katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Borno baada ya kushambulia mashamba yao, wakazi walisema Jumatatu.
Wiki iliyopita, wanamgambo hao waliua watu 25 na kujeruhi wengine kadhaa katika mashambulizi kwenye vijiji viwili katika jimbo la Borno, eneo linalokumbwa na uasi na kitovu cha uasi wa zaidi ya mwongo mmoja nchini Nigeria ambao ulienea katika nchi jirani za Chad na Cameroon.
Abubakar Masta, mkulima ambaye alinusurika, alisema washambuliaji Jumatatu nyakati za asubuhi walishambulia mashamba yao katika kijiji cha Kawuri na katika eneo la Konduga la serikali ya mtaa ya jimbo la Borno, wakiwa kwenye pikipiki na wakibeba bunduki.
Abubakar alisema “ Niliona maiti 10 za marafiki zangu waliochinjwa.
Wakazi wanashuku kwamba kundi la Boko Haram ndilo lilifanya shambulio hilo.