Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanamgambo wa Kiislamu waua raia 35 nchini Burkina Faso

90013 Bukinafaso+pic Wanamgambo wa Kiislamu waua raia 35 nchini Burkina Faso

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ouagadougou. Wanamgambo wanaoaminika wa Kiislamu wamewaua raia 35, kati yao 31 wakiwa wanawake katika shambulio katika ngome ya kijeshi na mji mmoja nchini Burkina Faso.

Inasemekana kuwa katika shambulio hilo, wanajeshi saba na wanamgambo 80 wameuawa baada ya jeshi kujibu mapigo juzi usiku katika eneo la Arbinda, kaskazini mwa jimbo la Soum.

Rais Roch Marc Christian Kaboré ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa.

Vikundi vyenye msimamo mkali vilianzisha mashambulizi nchini Burkina Faso na nchi nyingine za Afrika Magharibi kwa miaka ya karibuni na vimekuwa vikiendelea licha ya juhudi za mataifa ya magharibi kuzuia hali hiyo.

Novemba mwaka huu, askari 13 wa Ufaransa walikuwa baada ya helikopta kugongana katika operesheni dhidi ya wanamgambo kusini mwa Mali, karibu na mpaka na Burkina Faso.

Mwishoni mwa wiki, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron aligusia mapigano dhidi ya wanamgambo latika eneo la Sahel, alipotembelea Niger.

“Wiki zijazo zitaamua kuhusu mapigano yetu dhidi ya ugaidi,” alisema.

 

Shambulio la Jumanne liliendesha na makumi ya wapiganaji waliokuwa kwenye pikipiki na liliendelea kwa saa kadhaa.

 

Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulio hilo lakini makundi ambayo yanahusishwa ama na Al-Qaeda au Islamic State wanafanya mashambulizi ya kila mara katika eneo hilo.

“Hili ni shambulizi la kikatili lililosababisha mauaji ya raia 35,wengi wao wakiwa wanawake,” alisema Rais Kaboré katika taarifa yake. Pia alilipongeza jeshi la nchi hilo lililokabiliana na wanamgambo hao.

Mapema mwezi huu, takriban watu 14 waliuawa baada ya wauaji kufuatilia risasi watu waliokuwa kanisani mashariki mwa nchi hiyo.

Burkina Faso, nchi yenye wananchi wengi wa madhehebu ya Kiislamu, ilikuwa ya amani, lakini imeendelea kutetereka tangu mwaka 2015. Tangu wakati huo karibu watu 700 wameuawa na 560,000 kulazimika kuhama makazi yao.

Chanzo: mwananchi.co.tz