Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanamgambo 20 wa al-Shabab wauawa katikati mwa Somalia

Wanamgambo 20 Wa Al Shabab Wanamgambo 20 wa al-Shabab wauawa katikati mwa Somalia

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Taifa la Somalia kwa kusaidiana na washirika wa kimataifa wameangamiza magaidi 20 wa al Shabab katika operesheni ya usiku kucha wa kuamkia leo iliyofanywa katika eneo la kusini mwa mji wa Mudug wa katikati mwa Somalia.

Wizara ya Habari, Utamaduni na Utalii ya Somalia imetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, operesheni hiyo imewalenga magaidi wa al Shabab wakiwa katika maficho yao kwenye msitu wa Shabellow.

Taarifa ya leo Jumatatu ya wizara hiyo imesema: "Lengo la vikosi vya pamoja lilikuwa kuharibu mabehewa ya kivita yanayotumiwa na magaidi, shehena za kijeshi, chakula, dawa na kusambaratisha mtandao wao wote ambao umeharibiwa kabisa kwenye operesheni hiyo."

Aidha imesema, wanajeshi wa Somalia waliangamiza zaidi ya magaidi 100 wa al Shabab wiki iliyopita katika moja ya mapigano makali zaidi kuwahi kutokea tangu mwanzoni mwa waka huu na kufanikiwa kuwafurusha magaidi hao ambao wamekuwa wakivisumbua vikosi vya serikali karibu kila siku.

Hadi wakati tunaandika habari hii, genge la al Shabab halikuwa limetoa taarifa yoyote kuhusu mashambulizi hayo ya vikosi vya serikali dhidi yao.

Kampeni ya kurejesha udhibiti wa nchi inaendelea nchini Somalia baada ya serikali ya Mogadishu kuliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchelewesha kuondoka wanajeshi wa kigeni nchini humo.

Kwa mujibu wa ratiba ya hivi sasa, takriban wanajeshi 3,000 wa Misheni ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia walitakiwa kuondoka nchini humo mwishoni mwa mwezi uliopita wa Septemba na kuondoka kikamilifu ifikapo mwezi Disemba 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live