Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanakijiji wavamia kaka wawili kwa madai ya kuzuia mvua

0fgjhs601rv4nmj1b Wanakijiji wavamia kaka wawili kwa madai ya kuzuia mvua

Wed, 16 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wakazi wa eneo la Kibanga wanaamini kuwa kaka hao wana nguvu za kusababisha mvua na ukameHii ni baada ya kukatika ghafla kwa mvua wa masika mnamo Aprili kisha eneo hilo likaanza kushuhudia ukame Hali hii iliwachochea wakazi wa eneo hilo kupandwa na hasira na kuwavamia kaka hao wakiwalaumu kuwa chanzo cha masaibu yaoWawili hao, Odira Nyangwezo, 54, na Ooko Nyangwezo, 33, wanaripotiwa kukimbia makazi yao mnamo Jumamosi, Juni 12, usiku

Kaka wawili kutoka kijiji cha Kibanga, kaunti ya Homabay, wamekimbilia usalama wao baada ya wakazi kutishia kuwaua kwa madai kuwa ndio wamezuia mvua na kusababisha ukame unaoathiri eneo hilo.

Wawili hao, Odira Nyangwezo, 54, na Ooko Nyangwezo, 33, wanaripotiwa kukimbia makazi yao mnamo Jumamosi, Juni 12, usiku.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, Jumatano, Juni 16, wakazi wa eneo hilo wanaamini kuwa kaka hao wana nguvu za kusababisha mvua na ukame.

Hii ni baada ya kukatika ghafla kwa mvua wa masika mnamo Aprili kisha eneo hilo likaanza kushuhudia ukame.

Hali hii iliwachochea wakazi wa eneo hilo kupandwa na hasira na kuwavamia kaka hao wakiwalaumu kuwa chanzo cha masaibu yao.

Fauka ya hayo, wanakijiji pia walitishia kuwaua kaka hao wawili pamoja na familia zao nzima.

Wanakijiji waliandamana moja kwa amoja hadi nyumbani kwa kaka hao kuwavamia lakini tayari walikuwa wametoroka pamoja na familia zao.

Hivyo waliamua kuteketeza vifaa vyao vya nyumbani pamoja na maghala yao ya chakula.

Familia hiyo sasa inahofia usalama wao endapo wataamua kurejea manyumbani kwao.

Kwingineko buda mmoja aliyekuwa katika lojingā€™i mtaani Roysambu, Nairobi alitokwa na kijasho chembamba baada ya kisura waliyekuwa naye kutoweka na suti yake.

Inasemekana kwamba jamaa alikuwa amemchota mrembo huyo aliyekuwa na sura na umbo la kuvutia ambaye alikuwa akiwinda wanaume wenye pesa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke