Video inayovuma kwenye jukwaa la X ambayo zamani ilikuwa ya Twitter ambayo imepata hisia tofauti inanasa wakati wanajamii walipokusanyika kumkashifu maiti kwa kuwakata pesa zao kabla ya kujiua.
Kwa mujibu wa maelezo ya awali kabla ya kupata video hiyo, ilielezwa kwamba mwanamume huyo ambaye ni marehemu alifyonza mfuko wa hifadhi ya hela kwa ajili ya jamii.
Baada ya kumaliza pesa hilo kinyemela, jamaa huyo aliona kwamba atagundulika na kutakikana kulipa wakati uwezo wake wa kulipa ni finyu, na hivyo akaamua kujitoa uhai.
Kwa ghadhabu ya wanakijiji katika video hiyo, walimuandalia safari yake ya mwisho vyema lakini kabla ya kumfukia kwenye kaburi, waliamua kumpa funzo la mijeledi mikali kwa kufa na deni lao.
Katika video hiyo inayosambaa, jeneza la marehemu linaonekana kufunguliwa na wanajamii walijipanga wakiwa wamebeba fimbo mikononi mwao ili kumchapa mtu huyo. Kisa hicho kinaripotiwa kutokea katika kijiji kimoja nchini Angola.
Video hiyo ilishirikiwa kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa la microblogging na na nukuu;
"Alichota pesa za akiba ya jamii kisha akajiua baada ya kuzimaliza... hivi ndivyo wanavyompa funzo ... Angola"
Hata hivyo, ni vizuri kueleweka kwamba jamii nyingi hususani magharibi mwa Kenya, mtu ambaye amejitoa uhai kwa kitanzi, anatiwa mijeledi mikali kabla ya kutolewa, kama njia moja ya kukemea pepo ya kujinyonga.
Tukio hili lilikuwa tofauti kidogo na la kushangaza kwa sababu marehemu alichapwa kwa kufa na deni la watu katika jamii.