Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanakijiji 160 waliripotiwa kuvamiwa na kutekwa nyara Nigeria

Wanakijiji 160 Waliripotiwa Kuvamiwa Na Kutekwa Nyara Nigeria Wanakijiji 160 waliripotiwa kuvamiwa na kutekwa nyara Nigeria

Mon, 27 May 2024 Chanzo: bbc

Watu kumi wameuawa na takribani wanakijiji wengine 160 wametekwa nyara kutoka jamii ya mbali katika jimbo la kati la Niger nchini Nigeria, maafisa wanasema.

Idadi kubwa ya watu wenye silaha, wanaoshukiwa kuwa kutoka kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Nigeria Boko Haram, walivamia kijiji cha Kuchi Ijumaa usiku, afisa wa eneo hilo Aminu Abdulhamid Najume aliiambia BBC. Waliotekwa nyara wengi wao walikuwa wanawake na watoto, wakati waliouawa ni pamoja na wawindaji wa eneo hilo ambao walikuwa wakitoa ulinzi katika eneo hilo, alisema.

Inasemekana watu hao wenye silaha walipanda pikipiki hadi Kuchi na hata kutumia muda kupika chakula, kuandaa chai na kupora kabla ya kuondoka zaidi ya saa mbili baadaye.

Bw.Najume, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Maeneo ya Serikali ya Maeneo ya Munya, alisema jamii ya Wakurchi imeachwa na kiwewe na kuhangaika kusikia habari za waliochukuliwa.

Ikiandika kwenye mitandao ya kijamii, Amnesty International ilionesha "wasiwasi wake mkubwa" katika utekaji nyara huo mkubwa.

"Uvamizi wa kijiji na watu wenye silaha ni dalili nyingine ya kushindwa kabisa kwa mamlaka ya Nigeria kulinda maisha," ilisema.

"Tangu mwaka 2021 watu wenye silaha wamekuwa wakishambulia kijiji cha Kuchi kila mara na kuwabaka wanawake na wasichana katika nyumba zao.

"Mara kwa mara, watu wenye silaha wanadai mamilioni ya Naira kama fidia kutoka kwa watu ili kuepuka kutekwa nyara.

"Amnesty International inatoa wito kwa mamlaka ya Nigeria kukomesha visa hivi vya utekaji nyara na kuwafikisha washukiwa wahusika mbele ya sheria.

Utekaji nyara wa mara kwa mara na mauaji ni ushahidi wa wazi wa kushindwa kwa mamlaka kuwalinda watu." Mashambulizi katika jimbo la Niger yamezidi kuwa ya kawaida ingawa mara nyingi imekuwa haijulikani ikiwa watu wenye silaha wana uhusiano wowote na vikundi vya kijihadi.

Mwezi uliopita vijiji kadhaa vililengwa na magenge yenye silaha ya utekaji nyara ili kulipwa kikombozi.

Chanzo: bbc