Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wazichapa na Polisi

Police Msj.jpeg Wanajeshi wazichapa na Polisi

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), limesema linachunguza tukio la askari wa Jeshi hilo kuwashambulia kwa kipigo askari wa Jeshi la Polisi nchini humo, katika eneo la Kivuko cha Likoni, mjini Mombasa.

Hatua hiyo inafuata baada ya kusambaa kwa video iliyoonyesha Maafisa wa KDF wakizozana na Maafisa wa Polisi, mzozo ambao baadae ulionekana kwenda mbali zaidi baada ya Askari mmoja wa KDF kuonekana akimpiga Askari wa Jeshi la Polisi.

Jeshi hilo limesema linafuatilia kisa hicho ambacho kimeleta sintofahamu kwenye jamii, huku likisisitiza kuwashughulikia Askari wake wote watakaokutwa na hatia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live