Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wawarushia mabomu ya machozi waandamanaji

Sudan Waandamaji Wanajeshi wawarushia mabomu ya machozi waandamanaji

Mon, 18 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Sudan wamewafyatulia gesi za kutoa machozi waandamanaji wanaopinga mapinduzi katika mji mkuu, Khartoum jana.

Mji huo mkuu umekuwa eneo la maandamanao ya mara kwa mara tangu mkuu wa majeshi , Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, achukue mamlaka Oktoba mwaka jana, na kuchelewesha kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Vikosi vya usalama vilikuwa vimeweka vizuizi vya barabarani kwenye madaraja ya mto Nile yanayounganisha mji wa Khartoum na vitongoji vyake , kujaribu kuwazuia waandamanaji kukusanyika.

Mapema mwezi huu, Jenerali Burhan aliapa kutoa fursa utawala wa kiraia, lakini makundi ya upinzani yalipinga hatua yake, na kuitaja kuwa ni ya ujanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live