Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wavamia televisheni ya taifa Sudan

Sudan Coup Pic Data Wanajeshi wavamia televisheni ya taifa Sudan

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mshike mshike nchini Sudan, habari za hivi punde zilizotolewa na Wizara ya Habari na Mawasiliano nchini humo zinaeleza kuwa wanajeshi wamevamia makao makuu ya shirika la habari la taifa hilo kisha kuwashikilia baadhi ya watumishi mapema Oktoba 25, 2021.

Taarifa hiyo iliyotolewa kwa njia ya matando wa Facebook inaeleza kuwa kundi hilo kubwa la wanajeshi limevamia kituo cha televisheni pamoja na redio cha taifa kilichopo katika mji wa Omdurman.

"Kundi kubwa la Askari limevamia makao makuu ya TV na redio ya taifa yalipo Omdurman na kuwashikilia baadhi ya wafanyakazi" Imesema taaifa hiyo ya wizara.

Aidha kabla ya tukio hili mapema zaidi Oktoba 25, 2021 vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuhusu kuwekwa kizuizini kwa Waziri Mkuu pamoja mawaziri wengine wanne na Mwanachama mmoja wa chama tawala cha sovereign council.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live