Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi waua magaidi zaidi ya 180 Nigeria

Magaidi Nigeria Kifoooo.jpeg Wanajeshi waua magaidi zaidi ya 180 Nigeria

Sun, 3 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limeua zaidi ya magaidi 180 wanaoaminika kuendesha mashambulizi ya kigaidi katika kona mbalimbali za nchi hiyo.

Edward Buba, Msemaji Taifa wa Jeshi la Nigeria, amewaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja kwamba takriban watu wengine 204 wamekamatwa na mateka 234 wamekkombolewa kwenye operesheni za jeshi hilo.

Amesema: Idadi kubwa ya silaha na risasi zimepatikana kutoka kwa magaidi hao.

Vile vile amesema: Operesheni hizo ambazo zimelenga maeneo yanayotambuliwa kama ngome za wahalifu, zimeendeshwa kwa ushirikiano kati ya askari wa anga na wa nchi kavu katika mikoa mbalimbali ya Nigeria.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu pia, msemaji huyo wa Jeshi la Nigeria alisema kuwa, magaidi 31 wenye silaha wameangamizwa na wanajeshi wa Nigeria katika operesheni mbalimbali zilizofanywa na jeshi hilo katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika kwenye kipindi cha wiki moja.

Magenge yenye silaha yanafanya jinai nyingi dhidi ya wananchi wa Nigeria

Edward Buba alisema, wanajeshi hao waliwakomboa kwa uchache watu 10 waliokuwa wametekwa nyara na genge la kigaidi la Boko Haram na Daesh (ISIS) kwenye operesheni hiyo iliyofanyika kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Sehemu moja ya taarifa hiyo ilisema: "Jeshi, kupitia operesheni zake, linaendelea kushinda changamoto za uasi na ugaidi na lengo lake kuu ni kulinda nchi na kupambana na magenge yanayohatarisha amani na usalama na kukwamisha maendeleo ya taifa."

Mashambulizi ya kutumia silaha yamekuwa tishio kubwa la usalama katika mikoa ya kaskazini na katikati mwa Nigeria. Mashambulio hayo yamesababisha vifo na utekaji nyara wa watu wengi wasio na hatia katika miezi ya hivi karibuni.

Mwanzoni mwa mwezi ulioisha wa Novemba, maafisa wa polisi ya Nigeria walitangaza kwamba katika siku za hivi karibuni raia wasiopungua 40 wameuawa katika shambulio la magaidi wa Boko Haram kwenye jimbo la Yobe la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live