Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi watatu wa UN wauawa Mali

Makamanda Wakuu Wa Al Shabab Wauawa Na Vikosi Vya Somalia Wanajeshi watatu wa UN wauawa Mali

Tue, 21 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi watatu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameuawa na watano kujeruhiwa baada ya msafara wao kugonga kilipuzi katikati mwa Mali.

Taarifa ya vifo hivyo imetolewa leo Jumanne, Februari 21, 2023 na Umoja wa Mataifa katika kwenye ukurusa wao wa Twitter.

Mali inapambana kukomesha uasi wa kidini uliokita mizizi baada ya mapinduzi ya 2012 ambapo tangu wakati huo umeenea kutoka kaskazini mwa nchi hiyo mpaka Afrika Magharibi.

Maelfu ya watu nchini humo wamefariki dunia na mamilioni wakilazimika kuyahama makazi yao katika eneo lote la Sahel kufuatia vita hivyo.

Baadhi ya makundi yanayotajwa kuwa na uhusiano na Al Qaeda na Islamic State. Takriban walinda amani 281 wameuawa nchini Mali tangu kuanza kwa mkakati huo mwaka 2013, na kuifanya kuwa rekodi mbaya zaidi kwa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live