Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi waondolewa nyumbani kwa Bobi Wine

Habarileo Tz 143174621 257984679076173 3644365933396246799 N 660x375 Wanajeshi waondolewa nyumbani kwa Bobi Wine

Thu, 28 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Vikosi vya majeshi ya Uganda vimeondoka kwenye makazi ya kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu ‘Bobi Wine’ baada ya Mahakama nchini humo kuamuru kufanya hivyo siku tatu zilizopita.

Majeshi hayo yalikua yamezingira nyumba ya ‘Bob Wine’ na kumuweka kizuizini tangu Januari 14,2020.

Vikosi hivyo vya usalama viliweka kambi nyumbani kwa Bobi ‘Wine’ mara baada ya uchaguzi kwa kile walichodai kuwa ni kumlinda.

Uchaguzi huo mkuu wa Uganda, ulimpa ushindi Rais Yoweri Museveni, matokeo ambayo yamepingwa na ‘Bob Wine’ akidai kuwa uligubikwa na udanganyifu.

MAGARI SITA YA WIZI YAKAMATWA “TUMEMKAMATA KIMYAKIMYA MWIZI WA MAGARI WA DSM”

Chanzo: millardayo.com