Takriban wapiganaji sita wanaotaka kujitenga pamoja na wanajeshi wanne wameuawa katika mapigano ya siku chache zilizopita yaliyotokea kwenye eneo la wazungumzaji wa Kiislamu la kaskazini magharibi mwa Cameroon.
Duru za ndani za usalama na habari zilitangaza habari hiyo jana Jumatatu na kuongeza kuwa mapigano hayo yalitokea juzi Jumapili kati ya wanamgambo wanaopigania kujitenga na vikosi vya serikali ya Cameroon.
Afisa mmoja wa jeshi la Cameroon katika eneo hilo, ambaye aliomba jina lake lisitajwe amethibitisha habari hiyo na kusema: Siku ya Jumapili, wapiganaji wanaotaka kujitenga waliwavizia askari wa serikali waliokuwa kwenye doria katika eneo la Belo, na kuua askari watatu baada ya majibizano ya risasi.
Kwa mujibu wa afisa huyo na watu walioshuhudia ni kwamba, siku ya Jumamosi pia, kulitokea shambulio lingine la wanamgambo wanaotaka kujitenga katika mji wa Bamenda na kusababisha mauaji ya mwanajeshi mmoja wa serikali aliyejulikana kwa jina la Zambo Biyidi. Wanamgambo waanaopigania kujitenga nchini Cameroon
Shambulio hilo huko Bamenda lilitokea saa chache baada ya wanajeshi wa serikali kuvamia maficho ya watu wanaotaka kujitenga katika eneo la Nguri katika eneo hilo.
Sehemu moja ya matamshi ya afisa huyo inasema: "Magaidi sita wanaotaka kujitenga akiwemo kamanda wao waliuawa katika shambulizi hilo la kijeshi. Wengi wao walitoroka na majeraha ya risasi."
Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa, wapiganaji hao wanaotaka kujitenga wamekuwa wakifanya vitendo vya kigaidi dhidi ya raia, wakijihusisha na utekaji nyara kwa ajili ya kikomboleo.
Wanamgambo wanaopigania kujitenga eneo linalozungumza Kiingereza na lile linalozungumza Kifaransa wamekuwa wakipambana na vikosi vya serikali tangu mwaka 2017 katika mikoa inayozungumza Kiingereza ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Cameroon.