Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi waliotoweka Pwani ya Somalia wamefariki

Wanajeshi Marekani Wafa.png Wanajeshi waliotoweka Pwani ya Somalia wamefariki

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la maji la Marekani limetangaza kumalizika kwa zoezi la siku 10 la kuwatafuta na kuwaokoa maofisa wake wawili waliotoweka Pwani ya Somalia usiku wa tarehe 11 ya mwezi Januari.

Maofisa hao wa jeshi la maji la Marekani waliotoweka wakati wakijaribu kuizuia meli iliyokuwa imebeba silaha.

Mmoja wa wanajeshi hao aliripotiwa kuanguka kwenye maji kabla ya mwenzake kuruka ndani kwa jaribio la kumuokoa. Hakuna afisa alionekana tena baada ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamandi ya Marekani, baada ya kipindi cha siku 10 kuwatafuta maofisa hao, wamelazimika kuhitimisha zoezi hilo na kwamba hawajaweza kupatikana.Marekani inasema maofisa hao wamefariki

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa sasa huenda maofisa hao wamefariki na hatua ya kuopoa miili yao imeanza.

Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya kitengo kilichopewa majukumu ya kuzuia usafirishaji wa silaha katika pwani ya Somalia.

Uwepo wao kwenye eneo hilo hakujahusishwa na operation inayoendelea ya kulinda meli katika bahari ya shamu dhidi ya mashambulio ya waasi wa Houthi kutoka nchini Yemen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live