Wanajeshi wawili wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 15 katika mashambulio tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wahasiriwa wote walikuwa raia.
Haya yanajiri baada ya watu sita kujeruhiwa wakati wanajeshi waliporusha guruneti kwenye umati wa watu walipokuwa wakijaribu kuwakamata.
Afisa mmoja katika jimbo la Kivu Kusini alisema mwanajeshi aliyekuwa mlevi kwenye boti la Ziwa Tanganyika aliwaua abiria wanane wakiwemo watoto kabla ya kukamatwa.
Siku ya Jumapili mwanajeshi mwingine alimpiga risasi kanali mmoja, mlinzi wake na raia watano katika jimbo la Ituri.
Muuaji huyo ambaye pia inasemekana alikuwa mlevi, alipigwa risasi na mwenzake alipokuwa akikimbia.
Kwa zaidi ya miongo miwili watu kote mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamevumilia mashambulizi ya mara kwa mara na makumi ya makundi yenye silaha.
Rais FĂ©lix Tshisekedi amesema kukomesha ghasia hizo ni kipaumbele cha kwanza kwa serikali yake.
Majimbo mawili yalizingirwa kwa karibu mwaka mmoja uliopita.
Lakini ilikuwa na athari ndogo kwani waasi na wakati mwingine wanajeshi wa Congo wasio na nidhamu wanaendelea kusababisha uharibi