Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wafungwa jela kwa mauaji ya wanawake 

99aa4f8026b0cbed385a290baee4ddab Wanajeshi wafungwa jela kwa mauaji ya wanawake

Wed, 23 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAJESHI wanne wa Cameroon wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kutokana na kuhusika katika mauaji ya wanawake wawili na watoto wawili mwaka 2015.

Mauaji hayo yalinaswa kwenye kanda ya video ambayo ilisambazwa mitandaoni mwaka 2018 ikionesha jinsi waathirika hao walivyozibwa kwa kitambaa machoni na kupigwa risasi.

Serikali ya Cameroon awali ilikana na kusema video hiyo ni ya kughushi lakini baadaye ikawakamata wanajeshi saba.

Uchunguzi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Africa) ulionesha kuwa tukio hilo lilitokea katika kijiji kimoja cha mbali Kaskazini mwa Cameroon.

Katika video hiyo, maaskari wa jeshi wanaonekana wakiwatuhumu wanawake hao kwa kujihusisha na kundi la Wanamgambo wa Kiislamu ambalo mashambulio yake katika nchi jirani ya Nigeria yamesambaa na kuvuka mpaka.

Wahanga hao miongoni mwao akiwemo mtoto mchanga aliyekuwa amebebwa mgongoni na mmoja wa wanawake hao, walitembezwa kwenye barabara ya vumbi huku wakiwa wamefungwa macho kwa kitambaa na kisha kupigwa risasi mara 22.

Saba kati ya wale walioshitakiwa katika mahakama ya kijeshi ya Yaoundé, walifutiwa mashitaka huku wanne wakitiwa hatiani na kufungwa jela miaka 10 na ofisa mmoja akifungwa kifungo jela cha miaka miwili kwa kurekodi video ya tukio hilo na kuisambaza.

Awali, msemaji wa serikali alisema video hiyo ilirekodiwa nchini Mali na sare za kijeshi zilizooneshwa kwenye kanda hiyo sio zile zinazotumiwa na wanajeshi wa nchi hiyo katika eneo hilo la Cameroon.

Lakini ushahidi uliendelea kutolewa hali ambayo ilifanya kuwa vigumu kuficha.

Ni nadra sana kwa wanajeshi kufungwa kwa kuua raia nchini Cameroon.

Chanzo: habarileo.co.tz