Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Urusi wanaweza kupelekwa Burkina Faso - kiongozi wa kijeshi

Wanajeshi Wa Urusi Wanaweza Kupelekwa Burkina Faso   Kiongozi Wa Kijeshi . Wanajeshi wa Urusi wanaweza kupelekwa Burkina Faso - kiongozi wa kijeshi

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Burkina Faso anayeungwa mkono na jeshi amesema wanajeshi wa Urusi wanaweza kutumwa kupambana na wanajihadi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, iwapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.

Katika mahojiano, Ibrahim Traore alisema Urusi ilikuwa inatoa mafunzo ya vifaa na mbinu na iko tayari kuuza silaha zozote zinazohitajika na Burkina Faso.

Bw Traore alisema hakuna vizuizi kwa kile kinachoweza kununuliwa kutoka Urusi, Uchina, Uturuki au Iran, tofauti na nchi zingine.

Maoni yake yanawadia huku kukiwa na ripoti kwamba wapiganaji 100 wa Urusi wiki iliyopita walitumwa katika nchi hiyo ya Kiafrika kama wakufunzi wa kijeshi.

Maendeleo hayo pia yanachochea uvumi wa Burkina Faso kuimarisha uhusiano wa kiusalama na Urusi kama nchi jirani ya Mali, ambako mamluki wa Wagner wa Urusi wanaendesha shughuli zao.

Mahusiano ya nchi hiyo inayoongozwa na serikali ya kijeshi na Urusi yamekuwa yakipewa nadhari tangu ilipoondoa wanajeshi wa Ufaransa mapema 2023.

Burkina Faso imekuwa ikipambana na makundi ya kiislamu yenye mafungamano na al-Qaeda na Islamic State, ambayo yamechukua maeneo makubwa ya ardhi na kuwakosesha makazi mamilioni ya watu katika eneo kubwa la Sahel.

Chanzo: Bbc