Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Uganda na DRC waokoa watu w23 waliotekwa na ADF

E330F3E6 D5D8 4DCF A0C5 80E08E78AA32.jpeg Wanajeshi wa Uganda na DRC waokoa watu w23 waliotekwa na ADF

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Jumamosi walifanikiwa kuokoa watu wengine 23 waliotekwa nyara na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) katika operesheni yao ya pamoja ya kijeshi mashariki mwa DRC.

Meja Bilal Katamba, msemaji wa Idara ya Milimani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) amesema kuwa, jeshi hilo kwa kushirikiana na lile la DRC, wameendesha operesheni ya pamoja iliyopewa jina la "Shujaa," dhidi ya waasi wa ADF karibu na Mto Malibongo, kaskazini mwa Tokomeka mkoani Ituri, mashariki mwa DRC, na kufanikiwa kukomboa watu wengine wengi waliokuwa wametekwa nyara na waasi hao.

Amesema, mateka waliookolewa ni pamoja na wanawake 16 na wanaume saba, wamepokelewa katika makao makuu ya UPDF ya Luna, Mkoa wa Ituri, baada ya kuondolewa msituni na vikosi vya pamoja vinavyotembea kwa miguu.

Hawa ni baadhi ya mateka waliookolewa na kukabidhiwa kwa serikali ya DRC

Vilevile amesema: “Kati ya waliookolewa wako pia watoto 13 wakiweo watoto wachanga watatu chini ya mwaka mmoja ambao wana utapiamlo uliokithiri.”

Wanajeshi wa Uganda na wenzao wa Kongo walianza operesheni ya pamoja dhidi ya kundi hilo la waasi mwezi Novemba 2021, muda mfupi baada ya ADF kufanya mashambulizi ya mabomu huko Kampala, mji mkuu wa Uganda.

ADF ni kundi la waasi wa Uganda ambalo limejikita katika misitu ya mashariki mwa DRC. Kundi hilo la waasi linalaumiwa kwa kufanya ukatili mkkubwa na kusababisha uharibifu usiosemeka katika vijiji vya mashariki mwa DRC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live