Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Ufaransa wataondoka Niger ifikapo Disemba 22

Wanajeshi Wa Ufaransa Wataondoka Niger Ifikapo Disemba 22 Wanajeshi wa Ufaransa wataondoka Niger ifikapo Disemba 22

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: Voa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kuwa vikosi hivyo vitaondoka ifikapo mwishoni wa mwaka huu, ambapo kikosi cha kwanza kimeondoka nchini humo mwezi Oktoba. “Ifikapo Desemba 22, wanajeshi wote wa Ufaransa pamoja na vifaa vyao watakuwa wameondoka Niger”

Kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa wanaoshiriki katika operesheni ya kupambana na wanajihadi nchini Niger kutakamilika ifikapo Desemba 22, jeshi la nchi hiyo ya Sahel limesema Jumanne.

Watawala wa kijeshi wa Niger walifuta makubaliano ya ulinzi na Ufaransa, mshirika wake wa jadi wa usalama, wakati uhusiano ulipoharibika kufuatia mapinduzi ya mwezi Julai.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kuwa vikosi hivyo vitaondoka ifikapo mwishoni wa mwaka huu, ambapo kikosi cha kwanza kimeondoka nchini humo mwezi Oktoba. “Ifikapo Desemba 22, wanajeshi wote wa Ufaransa pamoja na vifaa vyao watakuwa wameondoka Niger” jeshi limesema katika taarifa.

Kuondoka kwao hadi sasa kumefanywa kwa njia iliyoratibiwa na salama, iliongeza. Kulingana na vyombo vya habari vya Niger, wanajeshi 1,346 wa Ufaransa na asilimia 80 ya vifaa vyao wameondoka, huku wanajeshi 157 pekee ndio wapo.

Chanzo: Voa