Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa RSF Sudan watangaza kusitisha mapigano kwa ajili ya Eid

Wanajeshi Wa RSF Sudan Watangaza Kusitisha Mapigano Kwa Ajili Ya Eid Wanajeshi wa RSF Sudan watangaza kusitisha mapigano kwa ajili ya Eid

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Usitishaji vita wa upande mmoja uliotangazwa na mkuu wa Kikosi cha jeshi cha Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan utaanza kutekelezwa leo kwa sababu ya sikukuu ya Waislamu ya Eid-al-Adha, itakayoanza Jumatano.

Kusitishwa kwa mzozo na jeshi la Sudan la RSF kulitangazwa katika rekodi ya sauti iliyotangazwa kwenye televisheni ya Al Arabiya na kiongozi wa RSF, Muhammad Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kama Hemedti.

Alisema hatua hiyo itatekelezwa Jumanne na Jumatano.

Jenerali Hemedti pia alilaani dhuluma zinazofanywa dhidi ya raia - ikiwa ni pamoja na zile zinazotekelezwa na vikosi vyake mwenyewe.

RSF imeshutumiwa kwa kuhusika na ukiukaji wa sheria huko Darfur.

Chanzo: Bbc