Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Nigeria waua magaidi 31 ndani ya wiki moja

Wanaigeria Magaidiiii Wanajeshi wa Nigeria waua magaidi 31 ndani ya wiki moja

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Magaidi 31 wenye silaha wameuliwa na wanajeshi wa Nigeria katika operesheni mbalimbali zilizofanywa na jeshi hilo katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Edward Buba, msemaji wa jeshi Nigeria ameseha hayo katika taarifa yake na kuongeza kwamba, magaidi wengine 81 pia wametiwa mbaroni na wanajeshi.

Msemaji huyo wa jeshi la Nigeria pia amesema: Wanajeshi hao waliwakomboa kwa uchache watu 10 waliokuwa wametekwa nyara na genge la kigaidi la Boko Haram na Daesh (ISIS) kwenye operesheni hiyo iliyofanyika kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema: "Jeshi, kupitia operesheni zake, linaendelea kushinda changamoto za uasi na ugaidi na lengo lake kuu ni kulinda nchi na kupambana na magenge yanayohatarisha amani na usalama na kukwamisha maendeleo ya taifa."

Mashambulizi ya kutumia silaha yamekuwa tishio kubwa la usalama katika mikoa ya kaskazini na katikati mwa Nigeria. Mashambulio hayo yamesababisha vifo na utekaji nyara wa watu wengi wasio na hatia katika miezi ya hivi karibuni. Wanajeshi wa Nigeria

Hii ni kusema kuwa, mwanzoni mwa mwezi huu wa Oktoba, askari 25 waliuawa katika shambulio la kuvizia lililofanywa na genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria.

Vyombo vya usalama vya Nigeria vilitoa taarifa na kutangaza kuwa, askari 20 wa nchi hiyo na watano wa jeshi la nchi jirani ya Chad waliuawa katika mapigano makali yaliyotokea kati yao na genge la Boko Haram ambayo yalipelekea pia kuangamizwa magaidi 47 wa genge hilo.

Genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram lilibeba silaha na kuanzisha uasi mwaka 2009 kwa lengo la kuasisi utawala eti wa Kiislamu kaskazini mwa Nigeria, ambapo mbali na ndani ya nchi hiyo, limepanua wigo wa mashambulio yake hadi katika nchi jirani za Niger, Chad na Cameroon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live