Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Niger wawataka wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo

Wanajeshi Wa Niger Wawataka Wanajeshi Wa Marekani Kuondoka Nchini Humo Wanajeshi wa Niger wawataka wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Kikosi tawala cha Niger kimeongeza maradufu matakwa yake ya kutaka wanajeshi wa Marekani waondoke, jambo ambalo ni pigo kwa maslahi ya usalama ya Washington katika eneo la Sahel.

Mwezi uliopita, kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdourahamane Tiani aliamuru wanajeshi wa Marekani kuondoka baada ya kumaliza makubaliano ya kijeshi.

Takriban wanajeshi 650 wa Marekani wamewekwa nchini Niger kufuatilia shughuli za wanajihadi.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, utawala wa Niger ulisema kuwa haujanufaika na mpango huo wa kijeshi wa Marekani kwani "uligeuka kuwa biashara ya kijinga".

Iliishutumu Marekani kwa kuinyonya Niger na kuingilia masuala yake ya ndani na kutaka kudhibiti uhusiano wake wa nje.

"Tunawezaje kuzungumza juu ya masilahi ya Niger, wakati Wamarekani walioko hapa wanakataa kutupatia viwianishi vya kambi za magaidi wanaotuomboleza kila siku?" taarifa hiyo ilisema.

"Tunawezaje kuzungumza juu ya maslahi ya Niger wakati Marekani hailipi hata kopeki moja [kitengo cha fedha cha Urusi] kwa Niger kwa kuweka majeshi yake kwenye eneo letu?"

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Pentagon zimepuuza kukataa kwa Niger makubaliano ya kijeshi, na kusema kuwa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili yanaendelea.

Kikosi cha kijeshi cha Niger awali kilionekana kuwa na msimamo mzuri na Marekani, lakini kimeelekea kwa Urusi baada ya kuvunja uhusiano na Ufaransa mwaka jana.

Chanzo: Bbc