Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Niger wauawa katika shambulio la kuvizia

Wanajeshi Wa Niger Wauawa Katika Shambulio La Kuvizia Wanajeshi wa Niger wauawa katika shambulio la kuvizia

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Wanamgambo wa kijihadi nchini Niger wamewaua wanajeshi 23 na kuwajeruhi wengine 17 katika mashambulizi kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, wizara ya ulinzi imesema.

Zaidi ya watu 100 waliokuwa na silaha wakiwa kwenye pikipiki walitumia vilipuzi na mabomu ya kujitoa mhanga kuvizia kitengo cha kijeshi kilipokuwa kikirejea kutoka kwa operesheni katika eneo la Tillabéri.

Wizara hiyo ilisema washambuliaji 30 waliuawa.

Kufuatia mapinduzi ya mwaka jana nchini Niger, watawala wa kijeshi wa nchi hiyo walikata uhusiano na washirika wake wa nchi za magharibi.

Vikosi vya Ufaransa vilivyokuwa vinaongoza mapambano ya kimataifa dhidi ya wanajihadi hao vililazimika kuondoka.

Wikiendi iliyopita mamlaka zilisema zinafuta makubaliano ya kuruhusu wanajeshi wa Marekani kuwa na makao yake nchini Niger.

Chanzo: Bbc