Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Marekani kuondoka Niger katikati mwa Septemba

Wanajeshi Wa Marekani Kuondoka Niger Katikati Mwa Septemba Wanajeshi wa Marekani kuondoka Niger katikati mwa Septemba

Mon, 20 May 2024 Chanzo: Bbc

Marekani na Niger wamekubaliana kwamba wanajeshi wa Marekani wataondoka nchini humo kabla ya Septemba 15," walitangaza katika taarifa ya pamoja siku ya Jumapili.

Walisema nchi hizo mbili "zimefikia makubaliano ya kujiondoa ili kutekeleza uondoaji wa vikosi vya Marekani, ambayo tayari imeanza".

Marekani imeitegemea Niger kama msingi wake mkuu wa kufuatilia shughuli za kikanda za wanajihadi.

Taarifa hiyo ilipongeza "kujitoa mhanga kwa pamoja kwa majeshi ya Niger na Marekani katika mapambano dhidi ya ugaidi".

Taarifa hiyo ilisema kujiondoa huko hakutaathiri kuendelea kwa uhusiano kati ya Marekani na Niger.

"Marekani na Niger zimejitolea kufanya mazungumzo ya kidiplomasia yanayoendelea ili kufafanua mustakabali wa uhusiano wao wa pande mbili," taarifa hiyo ilisema.

Mnamo mwezi Machi, Niger ilitangaza kumalizika kwa makubaliano yake ya kijeshi na Marekani. Msemaji wa jeshi Kanali Amadou Abdramane aliishutumu Marekani kwa kuleta pingamizi kuhusu washirika ambao Niger iliwachagua.

Kanali Abdramane aliishutumu Marekani kwa "mtazamo wake wa kudharau" na "tishio la kulipiza kisasi".

Mvutano uliongezeka kati ya Marekani na Niger baada ya rais mteule, Mohamed Bazoum, kupinduliwa mwaka jana.

Niger iko katika eneo la Sahel barani Afrika, ambalo linachukuliwa kuwa kitovu kipya cha kimataifa cha kundi la Islamic State.

Chanzo: Bbc