Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Eritrea waondoka Tigray

Gthynjkin Wanajeshi wa Eritrea waondoka Ethiopia

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi wa Eritrea waliokuwa katika jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopita wanaripotiwa kuondoka katika jimbo hilo ambalo limeshuhudia mzozo na mapigano kwa zaidi ya miakka miwili sasa.

Hayo yameelezwa na wakazi wa Jimbo la Tigray ambao wameziambia duru za habari kwamba, wanajeshi wa Eritrea wameanza kuondoka katika baadhi ya miji ya jimbo hilo linalokumbwa na vita. Awali wakazi wa Tigray walithibitisha kuyaona magari ya wanajeshi wa Eritrea yakiondoka katika miji ya Shire na Adwa, lakini wakasema kuwa, kuna baadhi ya wanajeshi hao waliobakia huko. Tangu yalipotangazwa makubaliano ya amani, serikali Ethiopia imesema imerudisha huduma nyingi muhimu huko Tigray lakini mamilioni ya watu katika eneo hilo bado wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu.

Vita kati ya vikosi vya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray vilizuka mwezi Novemba 2020 baada ya kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) kushambulia kambi za jeshi la shirikisho katika jimbo hilo. Wapiganaji wa kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF)

Ugomvi ulipungua baada ya pande hizo mbili kutia saini makubaliano mjini Pretoria na Nairobi mwezi Novemba mwaka jana. Mzozo wa Tigray umeua mamia ya maelfu ya watu huku mamilioni ya wengine wakilazimika kuhama makazi yao tangu mwezi Novemba 2020.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana 2022 imesema kuwa milioni 2.75 wamekimbia makazi yao kutokana na vita hivyo.

Mwezi uliopiita Ethiopia ilitangaza kwamba imeanza tena safari za ndege kuelekea Mekele, makao makuu ya jimbo la Tigray la kaskazini mwa nchi hiyo huku huduma muhimu pia zikianza tena katika jimbo baada ya miaka miwili ya mapigano makali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live