Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Afrika Kusini wauawa katika shambulio Mashariki mwa DRC

Wanajeshi Wa Afrika Kusini Wauawa Katika Shambulio Mashariki Mwa DRC Wanajeshi wa Afrika Kusini wauawa katika shambulio Mashariki mwa DRC

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini (SANDF) limethibitisha kuwa maafisa wawili wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika eneo la Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari SANDF limesema kuwa mojawapo ya kambi ya wanajeshi wa Afrika Kusini ilishambuliwa kwa bomu Februari 14 katika makabiliano ya moja kwa moja.

Maelezo kuhusu tukio hilo bado ni machache lakini waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali mjini Goma.

Wanajeshi hao ni sehemu ya kikosi cha walinda amani wa Jumuiya ya Maendeleao ya nchi zilizopo Kusini mwa Afrika(SADC).

Chanzo: Bbc